Wananchi washirikishwe katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Na. Dennis Gondwe, DODOMA NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago ametoa rai kuwa miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa wananchi washirikishwe kikamilifu ili wawe sehemu ya miradi hiyo na kusema kuwa utaratibu huo utaifanya miradi kudumu kwa muda mrefu. Kauli hiyo aliitoa alipoongoza Kamati ya Fedha na Utawala timu namba tatu kutembelea na kukagua umaliziaji wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Nguji iliyopo Kata ya Ng’hong’onha, jijini Dodoma. Alisema kuwa halmashauri inatekeleza miradi mingi ya maendeleo. “Nitumie nafasi hii kuwasisitiza kuendelea kuwashirikisha wananchi wa eneo husika kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Wananchi wakishirikishwa wanakuwa wamiliki wa mradi husika. Wasiposhirikishwa wanajiona siyo sehemu ya mradi. Hata kama kuna mtu anataka kufanya uharibifu kwenye mradi, wananchi wanabaki wanamtazama kwa sababu hawajashirikishwa. Nitumie nafasi hii kutoa rai, kwenye miradi yetu tunapoitekeleza, tuwashirikishe wananchi ...