Baraza la Madiwani la Jiji la Dodoma lapitisha Hesabu za Mwaka 2023/2024
Na. Valeria Adam, DODOMA Baraza la Madiwani la Jiji la Dodoma limefunga rasmi hesabu za mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2024, baada ya kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya ufungaji wa hesabu za halmashauri. Kwa mujibu wa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Jiji, CPA. David Rubibira alisema chanzo kikuu cha mapato ya halmashauri hiyo ni tozo, faini na ushuru mbalimbali. Mapato mengine yanatokana na michango ya afya, uwekezaji, pamoja na ruzuku kutoka Serikali Kuu, aliongeza. "Mapato na matumizi ya ndani ya halmashauri ni pamoja na mapato yenye tozo (kodi) ambayo ni kiasi cha shilingi bilioni 34.7, faini na tozo ni shilingi bilioni 2.6, Mapato mengineyo ni shilingi bilioni 6.6. Michango mengineyo ya afya ni shilingi bilioni 1.9, mapato yapatikanayo kwenye uwekezaji ni shilingi bilioni 5.5 na mapato toka serikali kuu ni shilingi bilioni 83.08 ambapo jumla ya mapato na matumizi yote ya ndani ya halmashauri ni shilingi bilioni 134.4" alisema CPA. Rubibira. Kwa upan...