Posts

Showing posts from January 19, 2024

Bazara la Madiwani Jiji la Dodoma lapitisha rasimu ya Mpango na Bajeti shilingi 146,287,642,299 kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limepitisha rasimu ya mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya shilingi 146,287,642,299.70 ikitajwa kuwa ni bajeti ya wananchi. Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Francis Kaunda akiwasilisha rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Akiwasilisha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Francis Kaunda alisema kuwa bajeti hiyo imelenga kutatua changamoto za wananchi. “Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmasahuri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ni jumla ya shilingi 146,287,642,299.70. Kati ya fedha hizo, shilingi 58,521,926,299.70 ni mapato ya ndani, shilingi 73,852,812,000 ni ruzuku ya mishahara, shilingi 1,168,778,000 ruzuku ya matumi...