Wananchi Kata ya Msalato watakiwa kufanya usafi kama utamaduni
Na. Mwandishi wetu, MSALATO Wafanyabiashara na wananchi katika eneo la Mnada wa Msalato wametakiwa kuufanya usafi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, badala ya kusubiri siku maalum za usafi. Wito huo ulitolewa wakati wa zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Samia Day , ambapo wananchi walishiriki kusafisha mazingira ya mnada. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Alicia Anthony, mchumi wa Kanda ya utoaji huduma Namba Sita ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma , alisema kuwa usafi ni muhimu sawa na chakula, hivyo wananchi wanapaswa kuuzingatia katika majumbani, maeneo ya kazi na biashara. “Mazingira safi humfanya mteja kujisikia salama na kuwa na imani na bidhaa au huduma anayopewa, niwapongeza wafanyabiashara kwa kushiriki zoezi hili na niwatake kulifanya kuwa utamaduni wa kila siku,” alisema Anthony. Kwa upande wake Balozi wa Mtaa wa Chikole, Joyce Jackson alisema kuwa wananchi wameitikia vizuri wito wa kufanya usafi katik...