Posts

Showing posts from April 24, 2025

Vijana waalikwa kushiriki Kongamano S/M Mbwanga

Image
Na. Mwandishi Wetu Vijana wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kujitokeza na kushiriki kongamano la vijana la Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 lenye lengo la kutoa elimu kuhusiana na fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo nchini. Mwenyekiti wa Kamati ya Kongamano la Vijana katika mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025, Abeid Msangi Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kongamano la Vijana katika mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025, Abeid Msangi akiongelea maandalizi ya kongamano hilo litakalofanyika katika Shule ya Msingi Mbwanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa kongamano hilo limeandaliwa kwa ajili ya vijana wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Nichukue nafasi hii kuwahamasisha vijana wa Jiji la Dodoma kujitokeza kwa wingi katika kushiriki kongamano hilo. Kongamano hilo linalenga kuwajenga vijana kuwa wazalendo, kuifahamu historian a falsafa ya Mwenge wa Uhuru. Pia tutatoa elimu kwa vijana kuhusiana na umuhimu wa kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa aman...

Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma atoa wito wananchi kujitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru, 2025

Image
Na. Leah Mabalwe, VIWANDANI Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Zainabu Abdallah amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 na kuushangilia katika maeneo yote utakapopita hasa katika Shule ya Sekondari Miyuji B utakapoweka jiwe la msingi shule hiyo. Aliyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2025. “Nipende kuwahamasisha wananchi wote wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 na kuukimbiza katika maeneo yote Jiji letu la Dodoma. Tunawategemea sana wananchi kwasababu Mwenge wa Uhuru ni mali yetu sote, tujitokeze na tushirikiane kuukimbiza katika maeneo yote” alisema Mwl. Abdallah. Alisema kuwa miongoni mwa miradi itakayotembelewa ni Shule ya Sekondari Miyuji B. Mwenge wa Uhuru utaweka jiwe la msingi ujenzi wa mabweni mawili, vyumba vinne vya madarasa na matundu 10 ya vyoo, aliongeza. Mwl....

Mradi wa kutengeneza Sufurua kutokana na taka za Aluminium utakaotembelewa na Mwenge wa Uhuru, 2025

Image
 

Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 04, Mabweni 02, Nyumba pacha ya Walimu, Matundu 10 ya Vyoo Shule ya Sekondari Miyuji

Image