Mkuu wa Mkoa wa Dodoma atembelea Kijiji cha Mitambo, Nanenane
Mkuu wa Mkoa, Rosemary Senyamule Agosti 7, 2025 ametembelea Kijiji cha Mitambo (Mechanisation Village) kilichosheheni teknolojia mbalimbali za kilimo cha umwagiliaji kinachopatikana katika Maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi maarufu kama Nanenane Kitaifa 2025 Kanda ya Kati yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini hapa. Vilevile, Senyamule akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, wametembelea mabanda kadhaa yakiwemo; Tume ya Ushindani, Chuo cha Biashara na Elimu (CBE), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Madini (STAMICO), VETA, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na TBA na kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hizo