Katambi: Vijana watakiwa kuyajua mema ya serikali
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewataka vijana wa Wilaya ya Dodoma kuyajua mema ya serikali ambayo ina neema kwa kila kijana nchini kuanzia aliyesoma hata ambae hajasoma. Akizungumza leo katika Kongamono la Vijana kuelekea mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 wenye Kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni yetu sote tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo’, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini. “Amini haujazaliwa kwa bahati mbaya, bali kwa kusudi la Mungu uliamliwa wewe uwe Mtanzania na sio nchi nyingine. Jambo la msingi ni kujitambua na kujua wajibu wako pia kujua wewe una ndoto gani na uzisimamie ndoto zako, na serikari inawajibu wa kuandaa mazingira wezeshi kwenu kwa sababu ni moja ya majukumu yake muhimu. Pia ni sehemu ya nne katika kukutengeneza wewe, Mungu kwanza, wazazi, jamii kisha serikali. Hivyo, fursa ni nyingi kwenu simamieni misimamo yenu na ajira zote ni zenu nyinyi vijana” alisema Katambi. “K...