Posts

Showing posts from December 14, 2024

Mbunge Mavunde akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa QADIRIA Orphan Centre

Image
 

RC Senyamule azindua Kampeni ya changia Damu jijini Dodoma

Image
 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma kwenye "Rudisha Tabasamu kwao Jogging"

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule mwenye kofia ya kimkakati katikati akiongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma kwenye "Rudisha Tabasamu kwao Jogging"

RC Senyamule akiongea na mamia ya wakazi wa Dodoma walioshiriki Jogging "Rudisha Tabasamu kwao" Chinangali Park

Image
 

Watoto kulindwa dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani Dodoma

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Rachel Balisidya amewataka wazazi kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha wanaweza kutimiza ndoto na malengo yao kwa kuzuia madhara yanayoweza kuwaharibia maisha kisaikolojia. Mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma ambae ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Rachel Balisidya akihutubia katika Tamasha la (TASHMEKU) Wito huo aliutoa leo alipomuwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma kwenye Tamasha la Tanzania Shiriki Malezi Endelevu Kupinga Ukatili (TASHMEKU) katika Shule ya Sekondari Dodoma Makulu kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto. Balisidya alisema kuwa Wilaya ya Dodoma bila ukatili inawezekana. Alisema kuwa ipo changamoto ya ukatili kwa watoto na asilimia kubwa ya ukatili inaanzia nyumbani kupitia baba, mama, mjomba, mwalimu na wale wanaowazunguka na kuwaharibu watoto kisaikolojia kwa kuwatesa, kubakwa na kuwanyim...

Wasimamizi miradi Jiji la Dodoma watakiwa kuwa wazalendo

  Na. Faraja Mbise, DODOMA Wasimamizi wa miradi ya ujenzi katika Shule ya Sekondari Matumbulu wametakiwa kuwa wazalendo na kutokwamisha juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.    Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Matumbulu iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Matamanio ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuleta hizi shule ni kwasababu watoto wasitembee umbali mrefu. Bado sisi Mkoa wa Dodoma tuna utoro na baadhi ya changamoto inayochangia utoro ni watoto kutembea mwendo mrefu kwenda shule. Kwahiyo, anaona fahari asiende shuleni. Lakini tuna ukatili wa kijinsia, kati ya maeneo ambayo watoto wanafanyiwa ukatili ni akiwa anaenda shuleni, wanapita maporini kwasababu ya umbali mrefu, yote haya Rais ametaka ayamalize kwa kuwajengea shule karibu na eneo lao” alisema Senyamule. Kwa upande wak...