Habitat for Humanity yaunga mkono usafi Soko la Sabasaba
Na. Mohammed Ramadhani, DODOMA Shirika la Habitat for Humanity Tanzania limeunga mkono juhudi za kuimarisha usafi katika Soko la Sabasaba jijini Dodoma kwa kutoa vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika shughuli za usafi wa mazingira. Mratibu wa shirika hilo, Elnoth Lekaaya alisema kuwa wameweza kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na Jiji la Dodoma katika kuhakikisha suala la usafi linafanyika kwa ufanisi katika maeneo ya jamii. Alisema kuw kupitia ushirikiano huo, shirika limechangia vifaa vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni moja, vikiwemo mifagio, reki, toroli na vifaa vingine mbalimbali. Lekaaya alisema kuwa msaada huo unalenga kuwawezesha wafanyabiashara na wadau wengine kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira ya soko, ili wananchi wanaofika kwa shughuli mbalimbali waweze kupata mazingira safi na salama. Aliongeza kuwa Habitat for Humanity Tanzania inatekeleza shughuli zake katika maeneo mbalimbali yanayolenga kuboresha maisha ya jamii, ikiwemo masuala...