Jiji la Dodoma latoa Kilo 790 za sukari kwa shule 150
Na. Faraja Mbise, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa kilo 790 za sukari kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na sekondari ili kuwawezesha kupata uhakika wa chai wanapokuwa shuleni ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini za kuhakikisha nishati safi ya kupikia inatumika katika taasisi mbalimbali. Kilo hizo zilitolewa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago wakati wa hafla ya ugawaji mitungi ya gesi na majiko 1,000 kwa shule, zahanati, vituo vya afya, vituo vya watoto yatima na mama na baba lishe tukio lililofanyika katika uwanja wa Nyerere square jijini Dodoma. Naibu Meya Chibago alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imechangia kilo 790 za sukari kwa shule za msingi na sekondari 150. Shule za msingi zilizopewa sukari hiyo ni 104 na shule za sekondari ni 46 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania na mbunge wa jimbo la Dodoma mjini, aliongeza. Akiongelea zoezi la utoaji wa majiko na mitungi...