Posts

Showing posts from October, 2026

Wananchi Kata ya Msalato watakiwa kufanya usafi kama utamaduni

Image
Na. Mwandishi wetu, MSALATO Wafanyabiashara na wananchi katika eneo la Mnada wa Msalato wametakiwa kuufanya usafi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, badala ya kusubiri siku maalum za usafi.   Wito huo ulitolewa wakati wa zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Samia Day , ambapo wananchi walishiriki kusafisha mazingira ya mnada. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Alicia Anthony, mchumi wa Kanda ya utoaji huduma Namba Sita ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma , alisema kuwa usafi ni muhimu sawa na chakula, hivyo wananchi wanapaswa kuuzingatia katika majumbani, maeneo ya kazi na biashara. “Mazingira safi humfanya mteja kujisikia salama na kuwa na imani na bidhaa au huduma anayopewa, niwapongeza wafanyabiashara kwa kushiriki zoezi hili na niwatake kulifanya kuwa utamaduni wa kila siku,” alisema Anthony. Kwa upande wake Balozi wa Mtaa wa Chikole, Joyce Jackson alisema kuwa wananchi wameitikia vizuri wito wa kufanya usafi katik...

Kizota yaadhimisha Samia Day, ikitoa elimu ya Lishe kwa Umma

Image
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA   Kata ya Kizota, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeadhimisha Samia Day kwa kutoa elimu ya afya na lishe kupitia Siku ya Afya na Lishe ya Mtaa (SALIKI), kufanya usafi katika Stendi ya Mnada Mpya, pamoja na kuwaelimisha wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika kata hiyo.   Akizungumza katika maadhimisho hayo, Polisi Kata ya Kizota, Inspekta Baraka Simbabawe alitoa elimu kuhusu umuhimu wa lishe bora, akitaja makundi muhimu ya vyakula kuwa ni nafaka na mizizi, jamii ya kunde, vyakula vinavyotokana na wanyama, mboga za majani na matunda. Alisema kuwa ulaji wa vyakula kutoka katika makundi hayo husaidia kujenga mwili na kuimarisha afya, huku lishe duni ikichangia changamoto kama utapiamlo, upungufu wa damu na mwili kukosa nguvu.   Inspekta Simbabawe aliwasisitiza wazazi kuhakikisha watoto wanapata chakula bora chenye virutubisho muhimu ili waweze kukua na kuimarika kiafya. Pia aliwahimiza wanawake wajawazito kuzi...