RC Senyamule afafanua uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura
Na. Asteria Frank, DODOMA Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa ufafanuzi wa dhana mbalimbali kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura unaoendelea katika Wilaya ya Dodoma, Chamwino, Bahi na Kongwa. Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule Kauli hiyo aliitoa alipokuwa mbele ya vyombo vya habari leo katika ukumbi wa mkutano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhusu juhudi za kuelimisha wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuhusu mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura unaoendelea katika Wilaya ya Dodoma, Chamwino, Bahi, na Kongwa. Alisema “napenda kutoa ufafanuzi kuhusu dhana mbalimbali zilizojengeka miongoni mwa wananchi. Kuna taarifa zisizo sahihi zinazozungumziwa kuhusu gharama za uandikishaji, muda wa vitambulisho vya kupiga kura na mchakato wa uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura”. Aliongeza kuwa uboreshaji taarifa za wapiga kura ni bure, wananchi hawatakiwi kulipa pesa yeyote katika mchakato huo. Dhana ya kwamba kuna gharama zinazohusi...