Posts

Showing posts from August 6, 2026

Teknolojia ya Kinengunengu mkombozi kwa vifaranga vya kuku Dodoma

Image
  Na. Mwandishi wetu, NZUGUNI Halmashauri ya Jiji la Dodoma limeibua ubunifu mpya wa teknolojia ya banda maalumu la kufugia vifaranga vya kuku maarufu kama ‘Kinengunengu’ linalolenga kuwasaidia wafugaji kupata njia bora ya kuwapatia vifaranga joto, chakula, malazi na mazingira salama ya ukuaji. Banda hilo limekuwa miongoni mwa vivutio vikubwa katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni kupitia banda la Jiji la Dodoma, ambapo wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujifunza namna ya kuanza na kuendeleza ufugaji wa kuku kwa njia rahisi na salama. Akielezea banda hilo, Afisa Mifugo wa Jiji la Dodoma, Delila Mlamka alisema kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakitegemea matumizi ya taa na mkaa kwa ajili ya kuwapatia vifaranga joto, lakini teknolojia ya Kinengunengu imekuja kuondoa utegemezi huo kwa kutumia muundo unaoweza kuhifadhi joto ndani ya banda. Alisema kuwa Kinengunengu kimeundwa katika mfumo wenye sehemu mbili muhimu, sehemu ya kul...

Silage suluhisho la uhaba wa chakula cha ng'ombe Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, NZUGUNI Wafugaji wa ng’ombe katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamehimizwa kuanza kutengeneza na kuhifadhi chakula cha mifugo kilichochachushwa (Silage) ili kuhakikisha mifugo inapata lishe ya kutosha wakati wa kiangazi, kipindi ambacho maeneo mengi hukumbwa na upungufu mkubwa wa malisho kutokana na ukame. Rai hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Delila Mlamka wakati akiwaelezea wananchi waliotembelea banda la mifugo la halmashauri hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini hapa. Alisema kuwa Silage ni chakula kinachotengenezwa kwa kuchanganya majani mabichi yaliyokatwakatwa, kiasi kidogo cha majani makavu, pumba na molases, kisha kuhifadhiwa kwenye mazingira yasiyoruhusu hewa ya oksijeni kuingia kwa siku 21 ili kichachuke vizuri na kuwa salama kwa matumizi ya mifugo. Alisema kuwa chakula hicho   kinaweza kutengenezwa kwenye mashimo au mapipa na kuhifadhiwa katika mifuko midogo ya plastiki na mifuko maalumu ya k...

City Boys na Royal Village Hotel waunga mkono Timu ya Dodoma Jiji kuelekea SHIMISEMITA

Image
  Na. Mwandishi wetu, DODOMA KAMPUNI ya uuzaji wa vifaa mbalimbali vya nyumbani na vyombo vya moto City Boys, kwa kushirikiana na Royal Village Hotel, imeendelea kuonesha mshikamano katika kuendeleza michezo kwa kuunga mkono Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwakabidhi jezi mbalimbali za michezo kuelekea mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA). Timu hiyo inayojipanga kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu jijini Mbeya, imekabidhiwa bibsi, jezi za mpira wa kikapu pamoja na jezi za mpira wa miguu, hatua inayolenga kuongeza hamasa, morali na ari kwa watumishi wanaoiwakilisha Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika mashindano hayo. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofayika ofisini kwake Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya City Boys, Patricia Olomi alisema kuwa wameamua kuunga mkono timu hiyo kwa kutambua nafasi ya michezo katika kujenga afya, mshikamano na kuongeza ufanisi wa watumis...