Posts

Showing posts from October 12, 2026

Watumishi watakiwa kuzingatia nidhamu na mshikamano kazini

Image
Na. Mwandishi Wetu, MAKOLE   Watumishi wa Jiji la Dodoma wametakiwa kuzingatia nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku lakini pia kuwa na mshikamano na ushirikiano katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuboresha utendaji kazi.   Hayo aliyasema Afisa Mtumishi Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Gerald Ruzika katika kikao cha kwanza cha Kamati Tendaji ya Wilaya ya Dodoma (TALGWU) kilichojadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Mei hadi Agosti 2026 kilichofanyika katika Ofisi ya Kata ya Makole.   Alisema kuwa nidhamu kazini ni msingi wa uwajibikaji na utoaji wa huduma bora, huku ushirikiano baina ya watumishi ukiwa njia muhimu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto na kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. “Nidhamu katika kazi na mshikamano miongoni mwa watumishi ni msingi wa utendaji wenye ufanisi. Tunapaswa kushirikiana katika kutatua changamoto ili kuimarisha uwajibikaji na kuboresha huduma tunazozitoa” alise...

Wananchi watakiwa kuzingatia taratibu za kupata Hati ya kusafiria Dodoma

Na. Coletha Charles, MNADANI   Wananchi wametakiwa kuzingatia taratibu na kuandaa nyaraka zinazohitajika wakati wa kuomba hati ya kusafiria nje ya nchi ili kurahisisha mchakato wa maombi na kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.   Wito huo umetolewa na Afisa Uhamiaji, Constable Asia Mussa, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALiKi) na Samia Day 2026, yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Jitegemee, Kata ya Mnanda, Jiji la Dodoma.   Alisema kuwa nyaraka zinazohitajika hutegemea shughuli za mwombaji na sababu za safari, akiwataka waombaji kuandaa vielelezo vinavyothibitisha utambulisho wao, shughuli wanazofanya na madhumuni ya safari.   “Ni muhimu mwombaji kuandaa nyaraka zinazohitajika kulingana na shughuli anazofanya na madhumuni ya safari yake ili kurahisisha mchakato wa maombi ya ‘passport’,” alisema Constable Mussa.   Alisema kuwa wafanyabiashara wanapaswa kuandaa fomu ya maombi ya hati ya kusafiria, kitambulisho cha t...

Wananchi wahimizwa kuzingatia mlo kamili kwa afya bora Dodoma

Image
Na. Coletha Charles, MNADANI   Wananchi wa Kata ya Mnadani wametakiwa kuzingatia ulaji wa mlo kamili wenye makundi sita ya chakula ili kuboresha afya, kuimarisha kinga ya mwili na kuhakikisha watoto wanapata virutubishi muhimu kwa ukuaji wao.   Wito huo umetolewa na Afisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Beatrice Moshi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Mtaa (SALiKi) na Samia Day 2026, yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Jitegemee, Kata ya Mnanda, Jiji la Dodoma.   Alisema kuwa wananchi wanaweza kupata lishe bora hata katika mazingira ya kipato kidogo kwa kupanga milo na kuchanganya vyakula vinavyopatikana katika maeneo yao yanayowazunguka.   “Makundi mbalimbali ya vyakula yana kazi tofauti mwilini, ikiwamo kutoa nguvu, kujenga mwili na kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa. Hivyo, ni muhimu kuyazingatia katika maandalizi ya milo ya kila siku,” alisema Moshi.   Aidha, aiongeza kuwa wazazi wanapaswa kuzingatia lishe ya wato...

Jamii yatakiwa kuimarisha ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili Dodoma

Image
Na. Coletha Charles, MNADANI   Wazazi na walezi wametakiwa kuimarisha usimamizi na malezi ya watoto ili kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kingono, unyanyasaji na changamoto za afya ya akili zinazohatarisha ustawi wa watoto katika jamii.   Wito huo umetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii, Aneth Mwambya wakati wa maadhimisho ya SALiKi na Samia Day 2026, yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Jitegemee, Kata ya Mnanda, Jiji la Dodoma.   Alisema kuwa malezi ya watoto ni jukumu la pamoja linalopaswa kuanzia katika familia, akibainisha kuwa shughuli za kutafuta maendeleo ya kiuchumi hazipaswi kuwafanya wazazi kupuuza usalama na mahitaji ya watoto wao.   “Malezi yanaanzia kwenye familia, wazazi tunapaswa kuzungumza na watoto, kuwapa mapenzi ya dhati, kuwafundisha maadili mema na kufuatilia mienendo yao badala ya kutegemea adhabu kali kila wanapokosea,” alisema Mwambya.   Aidha, aliongeza kuwa baadhi ya watoto wanakabiliwa na ukatili unaodaiwa kufanywa na w...