Posts

Showing posts from March 3, 2025

Wenyeviti wa mitaa Dodoma wahimizwa kutoa huduma bora

Image
Na. Halima Majidi, MTUMBA Wenyeviti wa mitaa jijini Dodoma wametakiwa kutambua na kusimamia majukumu yao ipasavyo kwa kuwapatia huduma bora na kuwashirikisha wananchi katika miradi mbalimbali ili kuleta tija katika ulinzi na utunzaji wa miradi hiyo. Hayo yalisema na Mwezeshaji wa Mafunzo ya Uongozi na Utawala bora, Mwinyipembe Victor, wakati akitoa mafunzo hayo kwa wenyeviti wa mitaa yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali Mtumba. Victor alisema kuwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ndogo ya 146 dhumuni la kuwepo kwa serikali za mitaa nikupeleka madaraka kwa wananchi, hivyo wenyeviti wa mitaa wanatakiwa kukumbuka na kutekeleza madaraka yao. ā€œWenyeviti wa mitaa tumekuwa tunajisahau sisi tunakuwa mabosi halafu wananchi wanakuwa wanahangaika, mwananchi atahangaika ndani ya miaka mitano ambayo umemnyanyasa ila ipo siku na wewe utahangaikaā€ alisema Victor. Aidha, aliwasitiza wenyeviti wa mitaa kutowaacha ny...