Posts

Showing posts from August 11, 2026

Makutupora kupata Zahanati Mpya, Mbunge wa Mtumba aweka nguvu kwenye ujenzi

Image
Na. Mwandishi wetu, MAKUTUPORA   Jitihada za kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Mchemwa zimepata nguvu baada ya kuchangiwa matofali 5,000, mifuko 250 ya saruji pamoja na gharama za mafundi hadi hatua ya kufunika jengo, huku wananchi wakihimizwa kushiriki kikamilifu kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika na kuanza kutoa huduma.   Mbunge wa Jimbo la Mtumba Anthony Mavunde alisema kuwa lengo la mchango huo ni kuhakikisha wananchi wa Makutupora wanapata huduma za afya karibu na makazi yao, akisisitiza kuwa ujenzi wa zahanati hiyo haupaswi kuwa jukumu la mtu mmoja, bali ni mradi wa wananchi wote.   “Zahanati si ya kwangu. Zahanati ni ya kwetu. Kila mmoja ahakikishe pale mchanga wake unaingia kwenye zahanati. Naomba mtoe ushirikiano. Kuna baadhi ya gharama si lazima nilipie mimi ila nguvu kazi yenu nayo inaweza kufanikisha jambo hili natamani kuwaona vijana wa hapa wakichapa kazi,” alisema Mavunde.   Mbunge huyo pia alisema kuwa anaamini serikali itaendelea kuu...