Kata ya Miyuji Yaongeza Kasi ya Usimamizi Wa Usafi wa Mazingira
Na. Manase Malima, MIYUJI Kata ya Miyuji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma imechukua hatua za kuimarisha usafi wa mazingira kwa kufanya ukaguzi wa vikundi vinavyohusika na ukusanyaji na uondoshaji wa taka, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha miji na majiji yanakuwa safi. Katika kutekeleza wito huo, wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha miji na majiji yanakuwa safi, Kata ya Miyuji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeelekeza nguvu katika kuboresha mfumo wa ukusanyaji na uondoshaji wa taka kupitia vikundi vinavyofanya shughuli hiyo katika mitaa ya kata. Leo tarehe 11 Septemba, 2026 Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Miyuji, ikiongozwa na Diwani wa Kata hiyo, Ringo Iringo, imefanya ukaguzi wa vifaa vinavyotumika katika shughuli za usafi, ikiwemo magari, na vifaa kinga kwa watendaji. Ukaguzi huo umehusisha kuangalia hali ya vifaa, mahitaj...