Vilabu vya michezo vyashiriki mazoezi ya viungo vya mwili jijini Dodoma
Na. Aisha Ibrahim, Mailimbili-DODOMA Vilabu mbalimbali vya michezo jijini Dodoma, vimejitokeza kwa wingi katika Bonanza la “Dodoma Aerobics Festival” msimu wa kwanza, lililofanyika katika kiwanja cha Chinangali Park, kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana kwa lengo la kuwakutanisha wanamichezo wote kushiriki mazoezi mbalimbali ya kuimarisha viungo vya mwili. Bonanza hilo liliandaliwa na kikundi cha wakufunzi wa michezo kutoka Jiji la Dodoma 'Dodoma Trainers Group' lilijumuisha mchezo wa kunyanyua uzito, kupasha mwili, kurukaruka na vikundi vya kukimbia. Akizungumza wakati wa bonanza hilo, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, aliwasisitiza wana Dodoma kuendelea kufanya mazoezi kila siku hasa siku ya Jumamosi kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alivyosisitiza kila mtanzania kujitengea siku ya kufanya mazoezi kwa lengo la kuimarisha viungo vya mwili. “Mazoezi ni afya, mazoezi ni tiba hi...