Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ni nyenzo ya utendaji kazi serikalini – Dkt. Biteko
Na. Mwandishi Wetu, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amehitimisha Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza lililofanyika jijini Mwanza akiweka mkazo kuwa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha kuwa kila taasisi inatimiza wajibu wake kwa ufanisi na hivyo kufikisha huduma bora kwa wananchi. Kutokana na hilo, Dkt. Biteko amewataka Wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini nchini kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu bila kuogopa kuchukiwa kwani taifa linawategemea ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi. “Hakuna mtu au taasisi inayoweza kufanikisha majukumu yake bila kufanya tathmini, ninyi ndio mnaoweza kutambua changamoto mapema na kuzitafutia suluhisho kabla hazijawa kubwa, taasisi yoyote inayokosa mfumo huu inafanana na timu inayoingia uwanjani bila refa..” alisema Dkt. Biteko. Alitoa mfano kuwa katika sekta ya umeme, kabla ya kupeleka huduma hiyo eneo lolote lazima tathmni ifanyike ili kuepuka kurudia...