Ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu wafikia 98%
Na. Dennis Gondwe, ZUZU UJENZI wa Kituo cha Afya Zuzu umefikia asilimia 98 ya utekelezaji kikitarajiwa kuhudumia wananchi 10,054 kwa kuwahakikishia huduma bora za afya na kuwaondolea hadha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya. Kauli hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Goodluck Magoti alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu kwa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Magoti alisema “kutokana na changamoto ya kukosa huduma za Kituo cha Afya katika Kata ya Zuzu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilianza ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu ili kusogeza huduma za matibabu mbalimbali karibu na wananchi. Halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi 299,439,348,54. Hadi kufikia sasa kiasi cha shilingi 285,4439,000,54 zimetumika kwa ujenzi wa majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara na kubakiwa na shilingi 14,000,348.54 kwa ajil...