Tofauti kati ya kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura na kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura
Na. Faraja Mbise, DODOMA Balozi wa Shina Namba Sita, Mtaa wa Chang’ombe katika Kata ya Ihumwa, Adawila Zakayo alipokuwa akifafanua kwa wananchi tofauti ya zoezi la kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura na kujiandikisha katika orodha ya mpiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Zoezi la kuhakiki na kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura lililofanyika tarehe 25 Septemba, 2024 hadi Oktoba 1, 2024 lilimtaka mwananchi kwenda kuboresha taarifa zake katika daftari la kudumu la mpiga kura tofauti na zoezi la sasa ambalo linamtaka mwananchi kujiorodhesha katika orodha ya mpiga kura lililoanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba, 2024 linalohitaji mwananchi kwenda kuandikishwa kwenye orodha ya mpiga kura kwa lengo mahususi kabisa la kuchagua viongozi ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa. Ufafanuzi huo ulitolewa na Balozi wa Shina Namba Sita, Mtaa wa Chang’ombe katika Kata ya Ihumwa, Adawila Zakayo alipokuwa akifafanua kwa wananchi tofauti ya zoezi ...