AI Ultrasound kuokoa maisha ya Mama na Mtoto Dodoma
Na. Lulu Luvanda, MKONZE Mkoa wa Dodoma umechaguliwa kuwa mkoa wa majaribio katika matumizi ya teknolojia ya AI Ultrasound, kupitia Mradi wa The Study of AI-Facilitated Ultrasound Feasibility and Assessment of Resources and Integration (SAFARI Project), unaolenga kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. Hatua hiyo imekuja wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya AI Ultrasound kwa vituo 32 vya kutolea huduma za afya katika Mkoa wa Dodoma, iliyofanyika katika Kituo cha Afya Mkonze, jijini Dodoma. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alikipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kuendelea kufanya tafiti zenye uhalisia na zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, ikiwemo tafiti katika sekta za Utalii, Mazingira pamoja na Lishe. Alisema kuwa matumizi ya vifaa hivyo katika vituo vya afya yatawezesha wananchi kupata huduma za awali kwa ukaribu zaidi, hivyo kupunguza changamoto ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za uchunguzi...