WAFUGAJI DODOMA WASHAURIWA KULIMA MALISHO

Na. Dennis Gondwe, NANENANE- ZUGUNI WAFUGAJI katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufanya ufugaji wa ndani na kulima malisho ya mifugo ili kujihakikishia kipato. Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mchomvu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari walipotembelea Banda la Mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane eneo la Nzuguni jijini Dodoma. Mchomvu alisema “tunahimiza wafugaji kufanya ufugaji wa ndani. Hivyo, ni muhimu mfugaji alime malisho yake kwa ajili ya kujiongezea kipato na tija ya maziwa na nyama. Wakati mwingine tunawafundisha ambao siyo wafugaji kulima malisho kama zao la biashara. Dodoma upatikanaji wa majani ni mgumu hivyo, mtu anaweza kulima malisho kama zao la biashara akayakata akayaanika na kuyafunga katika mfumo wa bezi na kuwauzia wafugaji. Na soko lipo wazi kabisa kwa wafugaji na bei ni nzuri beli moja tunalipata kwa shilin...