Posts
Showing posts from April 1, 2025
Serikali yatoa fedha kujenga Kituo cha Jemolojia ili kuongea thamani ya Madini
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa katika kuhakikisha Madini yanaongezewa thamani kabla ya kupelekwa nje ya nchi, Serikali imetoa fedha nyingi na kujenga Kituo kikubwa cha Jemolojia ili kuwa na kituo bora, chenye mashine bora na wataalam bora nchi nzima ili kuhakikisha Madini hasa ya vito yanaongezewa thamani hapa nchini kwa viwango vinavyohitajika kabla ya kusafirisha kwenda nje. Mhandisi Samamba aliyasema hayo jijini Dodoma katika hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano kati ya Kampuni Sun Set kutoka Tailand na Taasisi ya Jemolojia Tanzania iliyoko chini ya Wizara ya Madini. Alisema kuwa watahakikisha kwamba wanaweka utaratibu wa namna ambavyo makubaliano hayo yatatekelezwa ili pande zote mbili waweze kunufaika na makubaliano hayo. āKupitia Kituo chetu chetu cha TGC, Mheshimiwa Rais ameweka fedha nyingi, tumejenga jengo kubwa kabisa ambacho ni kituo kikubwa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla ambapo lengo...