Wanasheria waanza mwaka mpya wa Mahakama
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua rasmi mwaka mpya wa Mahakama 2024 na kuwatakia wanasheria wote kheri ya mwaka mpya wa mahakama ulioanza Februari 1, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama ya Rufaa Kauli hiyo aliitoa katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika bustani ya mapumziko Chinangali jijini Dodoma. āTunaanza rasmi mwaka wa Mahakama na tunawakumbusha kuwa na mchango katika utendaji kazi kwa wadau wote wa Mahakama nchini, na nawakumbusha kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyenu vya utendaji kazi mlivyo viapa wakati wa kuanza kazi hiiā alisema Dkt. Samia Suluhu Hassan. Aidha, aliongezea kwa kuwapongeza watumishi wote wa Mahakama kwa kufanya kazi nzuri kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao. āNawapongeza sana waheshimiwa Mahakimu, wasajili wa mahakama kuu, majaji wa mahakama za rufaa na watumishi ...