Posts

Showing posts from March 5, 2026

Jiji la Dodoma kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Image
 

Wanawake watakiwa kulipa kodi na kukuza uchumi katika Jiji la Dodoma

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wanawake wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, hususan wafanyabiashara na wajasiriamali, wametakiwa kuendelea kulipa kodi na tozo kwa wakati ili kuchangia maendeleo ya jiji pamoja na kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla. Wito huo ulitolewa na Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Zuzu, Pilly Hassan, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 8 Machi, 2026. Alisema kuwa ulipaji wa kodi ni moja ya njia muhimu inayosaidia serikali   kupata mapato ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu ya masoko, barabara na huduma nyingine muhimu kwa wananchi. “Wanawake wengi wa Jiji la Dodoma tunajishughulisha na shughuli za biashara na ujasiriamali. Hivyo, tunapaswa kuwa mfano mzuri kwa kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu wa kulipa kodi na tozo za serikali kwa hiari na kwa wakati. Kupitia kodi hii itaweza kutusaidia mambo mbalimbali na ya muhimu kama vile kujeng...