Posts

Showing posts from October 17, 2024

Elimu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inaendelea

Image
 

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wafanyabiashara wamo

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wafanyabiashara Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamehamasishwa kujitokeza kushiriki katika mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili kupata viongozi walio bora ambao wanatambua wajibu wao ili kuwawezesha wafanyabiashara kutatua changamoto zao katika biashara. Meneja wa Hoteli ya Spring Hills, William Mndeme akielezea umuhimu wa wafanyabiashara kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Rai hiyo ilitolewa na Meneja wa Hoteli ya Spring Hills, William Mndeme alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wafanyabiashara kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Meneja Mndeme aliwashauri wafanyabiashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuitikia wito wa kwenda kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi walio bora na wenye manufaa katika kukuza uchumi wa nchi. “Ili tuweze kufanya biashara vizuri, lazima tuwe na viongozi bora na viongozi wanaotambua wajibu wao...

Wafanyabiashara Dodoma washauriwa kujiandikisha orodha ya wapiga kura

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wafanyabiashara wameshauriwa kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kupiga kura kwa kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ili waweze kupiga kura na kuwachagua viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Meneja wa Kidia Vision Hotel, William Moshi Ushauri huo ulitolewa na Meneja wa Kidia Vision Hotel, William Moshi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wafanyabiashara kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ili kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa nje ya hoteli yake. Moshi ambae ni moja ya wafanyabiashara maarufu alisema kuwa anawahamasisha wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kujitokeza kushiriki zoezi la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura. Kupiga kura ni haki ya msingi ya kikatiba. Wananchi watumie fursa hiyo kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa ili kuepukana na madhara yote yatakayojitokeza pindi wasipojiandikisha katika orodha ya wapiga kura na kushindwa kuwachagua viongozi bora. “Nawasihi wakazi wot...

Ujenzi Ofisi ya Machinga Mkoa wa Dodoma

Image