WILAYA YA DODOMA ILIKUSANYA 44,454,939,022 MWAKA 2022/2023

Na. Dennis Gondwe, DODOMA WILAYA ya Dodoma ilikusanya mapato ya shilingi 44,454,939,022 kupitia mifumo ya kieletroniki na kutekeleza miradi ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2022/2023. Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Chamwino jijini hapa. Ukusanyaji wa k odi na m apato kwa mfumo wa TEHAMA umeendelea kuimarika. “ Mheshimiwa Rais; w ilaya kwa mwaka wa fedha 2022/ 20 23 ilifanikiwa kupata m ashine za kielektroniki za kukusanyia mapato ( POS ) 304 na shilingi 44,454,939,022.82 zilikusanywa na kutumika kwenye miradi ya maendeleo ” alisema Mbugi . Kuhusu sekta ya biashara alisema malipo yote yanafanyika kupitia benki. “ Mheshimiwa Rais; Wilaya ya Dodoma imefanikiwa kusajili wafanyabiashara kwenye mfumo wa s erikali za m itaa wa ukusanyaji m apato na mali...