Mikopo ya asilimia 10 yawang’arisha wajasiriamali Makutupora
Na. Nancy Kivuyo, MAKUTUPORA Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia utoaji wa mikopo ya asilimia 10 yanufaisha makundi ya wanawake katika kujikwamua kiuchumi katika Kata ya Makutupora ikitajwa kuwa chachu ya kuinua maendeleo katika sekta ya kilimo, ufugaji na ujasiriamali. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na makundi ya wanawake waliopata mikopo ya asilimia 10 katika Kata ya Makutupora, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Makutupora, Andrew Boma alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kusimamia vema uwezeshaji wa wananchi kupata haki zao hasa kwa makundi maalum ambayo yamewezeshwa kupitia mikopo hiyo. “Sisi Kata ya Makutupora vikundi 20 vimepatiwa mkopo wa jumla ya shilingi 230,000,000. Vikundi vya wanawake ni 10, vijana saba na watu wenye ulemavu vitatu. Mpaka sasa wameweza kurejesha shilingi 159, 980,000 na bakaa inaendelea kulipwa na vikundi hivyo” alisema Boma. Aliongeza kuwa vikundi hivyo vinajishughulisha na shughuli mbalimbali kama...