JIJI LA DODOMA LAPELEKA MIL. 20,000,000 KUMALIZIA MAABARA

Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KUSINI HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepeleka shilingi 20,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la maabara katika Shule ya Sekondari Wella iliyopo Kata ya Kikuyu Kusini. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo katika hafla fupi ya kupokea vifaa vya maabara vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini. Kayombo alisema “Mheshimiwa mbunge hapa tayari unaona ujenzi unaendelea kwenye maabara yetu kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, na sisi hatuwezi kukuangusha kwa sababu tunafanya kazi kwa kushirikiana. Tumeshaleta shilingi 20,000,000 hapa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara na inaenda kumaliziwa. Tunataka wanafunzi wetu waweze kufanya majaribio ya sayansi kwa vitendo. Mheshimiwa mbunge kwa maelekezo yako ya juzi ulituelekeza tutafute fedha na tumeshapata shilingi 8,000,000 kwa ajili ya kukamilisha matundu saba ya vyoo. Miongoni mwa changamoto am...