KISASA SEC YANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA RAIS, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Na. Dennis Gondwe, DODOMA SHULE ya Sekondari Kisasa ni mnufaika wa uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu na kuchangia kuongeza kiwango cha ufaulu. Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisasa, Mwl. Fredy Nyandoro alipokuwa akisoma taarifa ya shule Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisasa, Mwl. Fredy Nyandoro alipokuwa akisoma taarifa ya shule hiyo katika Mahafali ya 15 ya kidato cha Nne ya shuleni hapo. Mwl. Nyandoro alisema “ndugu mgeni rasmi, shule yetu tumekuwa na mafanikio kadhaa tangu kuanzishwa mwaka 2006. Mafanikio hayo ni kuongeza ufaulu mwaka hadi mwaka, kuongeza idadi ya watahiniwa na idadi ya vijana wanaojiunga elimu ya juu na vyuo vya kati imeongezeka. Shule imefanikiwa kuongeza miundombinu mwaka 2019 tulianza kujenga jengo la utawala na limekamilika. Mwaka 2021 tukapata mradi wa kuongeza madarasa kwa fedha za Uviko- 19 tulikuwa na madarasa matatu na kufanya madarasa kufikia ...