Wasimamizi vituo vya kupigia kura watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Na. Dennis Gondwe, MTUMBA WASIMAMIZI wa vituo vya kupigia kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na uzalendo wakizingatia kanuni na taratibu ili kuweza kufanikisha uchaguzi huo. Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Dkt. Frederick Sagamiko wakati akifungua semina Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali Mtumba. Dkt. Sagamiko alisema kuwa wasimamizi hao wapo kwa ajili ya kuapishwa na kupewa mafunzo kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutokana na sifa na uwezo wao katika utendaji kazi ndiyo zimewafanya waweze kuchaguliwa. “Tunahitaji kuongeza umakini na usikivu wakati huu wa mafunzo. Hata kama ulisimamia uchaguzi uliopita, huu ni wa mwaka 2024 na haujawahi kufanyika popote. Hivyo, kuna utofauti kati ya...