Posts

Showing posts from June 8, 2026

Vita dhidi ya Mbegu feki vyazaa matunda

Image
Na. Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma Serikali imeendelea kuimarisha hatua za kudhibiti na kutokomeza tatizo la mbegu feki nchini kupitia mifumo ya kisasa ya uthibitishaji wa ubora, ukaguzi wa mara kwa mara na utoaji wa elimu kwa wakulima. Akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Onesmo Merdson Mnkondya, kuhusu mpango wa Serikali wa kukomesha mbegu feki nchini, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amesema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha Sheria ya Mbegu (Sura ya 308, Toleo la Urekebu la mwaka 2023), mbegu zote zinazouzwa nchini zinapaswa kuthibitishwa ubora wake na Taasisi ya Uthibitishaji wa Mbegu Tanzania (TOSCI). Silinde aliaema kuwa TOSCI imeanzisha matumizi ya lebo za kielektroniki zinazotolewa kwa kampuni za mbegu ili kuwasaidia wakulima kuhakiki uhalisia wa mbegu wanazonunua. Kupitia mfumo huo, mkulima anaweza kukwangua lebo maalum iliyowekwa kwenye kifungashio cha mbegu na kuingiza namba husika kwenye simu yake ya mkononi ili kupata taarifa za uthibitisho wa mbegu h...

Waziri Mavunde akabidhi vifaa vya Michezo UMISETA Dodoma

Image
  Na. Mwandishi wetu, DODOMA Wanafunzi wanaojiandaa kushiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) ngazi ya mkoa wamepata hamasa mpya baada ya kupokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtumba na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Vifaa hivyo vilikabidhiwa katika Shule ya Sekondari Dodoma kwa niaba ya Mbunge huyo kupitia Katibu wake, Silas Makanyaga, ambae alisema kuwa Jiji la Dodoma kupitia Ofisi ya Afisa Elimu Sekondari liliwasilisha ombi la vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya UMMISETA ngazi ya wilaya na mkoa, ambapo Mbunge amejitoa kusaidia kwa kununua jezi kwa kila mchezo. “Tunawaomba vijana wetu kucheza kwa nidhamu, kuwasikiliza walimu wao na kuendelea kufanya vizuri kama ilivyo desturi ya Jiji la Dodoma ambalo limeendelea kuwa kinara kwa ushindi wa makombe mbalimbali” alisema Makanyaga. Kwa upande, Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma, Mwl. Daniel Mapilya alisema kuwa tayari wanafunzi 120 kuto...