Prof. Kabudi atoa salam za pongezi kwa wataalam walioshiri kutengeneza Sheria ya Mazingira
Na. Nancy Kivuyo, Dodoma Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Prof. Palamagamba Kabudi amewasihi viongozi wenye mamlaka ya kusimamia Sheria ya Mazingira ngazi zote kuziweka katika utekelezaji ili utunzaji wa mazingira ufanikiwe kwa asilimia zote. Aliyasema hayo wakati akitoa salamu katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete. Prof. Kabudi alisema kuwa utunzaji wa mazingira ni jambo mtambuka wananchi wote wanapaswa kulifahamu. Aliomba pia kuwatambua wataalam waliohusika katika utengenezwaji wa Sheria ya Mazingira. “Mheshimiwa Makamu wa Rais, na viongozi mliopo hapa, mimi pamoja na wataalam wa sheria tulishiriki mchakato wa kuandaa Sheria ya Mazingira ambao ulikua na safari ndefu, lakini tunashukuru tulifanikiwa kwa kiwango kikubwa na leo tupo hapa. Nawapongeza sana japokuwa kuna wenzetu kwa isivyo bahati wametangulia mbele za haki” alisema Prof. Kabudi. Aliongeza kuwa baada ya kuandaa sheria ile kish...