TARURA Dodoma yatakiwa kukamilisha miradi kwa wakati
Na. Coletha Charles, NZUGUNI Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wametakiwa kukamilisha kwa wakati, miradi ya uboreshaji wa barabara yenye urefu wa kilomita 3.8 kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha ili iweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi wa Jiji la Dodoma. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo, ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabiliana na athari za mvua za El Nino. Alisema kuwa utekelezaji wa mradi huyo unapaswa kwenda sambamba na usimamizi madhubuti wa muda, ubora wa kazi na matumizi sahihi ya fedha, ili wananchi wa Jiji la Dodoma wanufaike na miundombinu hiyo kwa muda uliokusudiwa. “Ninawasihi TARURA kuhakikisha mradi huu unakamilishwa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa, ili wananchi waweze kupata manufaa yaliyokusudiwa. Muhimu ni kuhakikisha fedha zinazotumika katika mradi huu zinatoa thamani halisi kwa wanan...