KLINIKI YA ARDHI JIJI LA DODOMA YAHUDUMIA WANANCHI 3,056 NDANI YA SIKU 5

Na. Dennis Gondwe, DODOMA KLINIKI ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma imehudumia wananchi 3,056 waliokuwa na kero za muda mrefu kuhusiana na sekta ya Ardhi yakiwa ni mafanikio makubwa kwa wananchi wengi kuhudumiwa kwa muda mfupi. Mkurugenzi wa Jiji, John Kayombo Takwimu hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake. Kayombo alisema “zoezi hili limetoa matokeo chanya kwa ujumla. Wananchi 3,056 walisikilizwa. Hati 1,474 zilitolewa papo hapo. Maombi mapya ya hati 561 yalipokelewa, namba za malipo 1,674 zilitolewa, viwanja 645 vilipandishwa kwenye mfumo, migogoro ya ardhi 774 ilisikilizwa, wananchi 149 walipata huduma za Mipango Miji na wananchi 221 walipata huduma za upimaji” alisema Kayombo. Akiongelea kliniki hiyo, alisema kuwa ililenga kutatua changamoto za Ardhi kwa haraka. “Zoezi hili ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa mkakati wa Mkoa wa Dodoma wa kumaliza changamoto za Ard...