Msalala DC wajifunza mbinu za ukusanyaji mapato kupitia mfumo wa kanda Dodoma Jiji
Na. Mwandishi Wetu Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imetembelea Ofisi ya utoaji huduma Kanda Namba Moja iliyopo Soko la wazi la Machinga, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ili kujifunza mbinu za ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo wa kanda ambao umesaidia kuongeza ufanisi wa makusanyo na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Akielezea namna ya utendaji kazi wa kanda hiyo, Nicholaus Mitembo, Meneja wa Kanda Namba Moja, alisema kuwa kanda hiyo inatoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara na kuwahamasisha kulipa mapato kwa hiari na kwa wakati ili kuepuka adhabu na pia kuchangia maendeleo ya eneo lao. Aidha, alisema kanda hiyo inatarajia kukusanya mapato ya shilingi 19,162,421,314.32. Nae, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Rose Manumba, aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kukubali na kutoa nafasi ya kujifunza katika halmashauri hiyo. Aidha, aliwakaribisha viongozi na watumishi wa jiji hilo kutembelea Msalala kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu shughuli kuu za k...