Posts

Showing posts from September 4, 2024

Juhudi na nidhamu yatakiwa kwa washiriki wa mafunzo ya Jeshi la Akiba Dodoma

Image
Na. Rahma Abdallah, MPUNGUZI Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri amewataka washiriki wa mafunzo ya Jeshi la Akiba kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa muda wote wa mafunzo na kuzingatia yote watakayo fundishwa ili kuwa kuwa askari mahili. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri akifungua mafunzo ya Jeshi la Akiba Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya 17 ya Jeshi la Akiba Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari Mpungunzi iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema kuwa wakufunzi wa mafunzo hayo wanauzoefu mkubwa utakaowasaidia kuimarika katika kozi mbalimbali za jeshi la akiba. “Niwaase mfuate maelekezo, mfuate mafunzo yote ya medani, mafunzo ya kitendaji, pia kuwa na nidhamu wakati wote wa mafunzo. Msingi mkubwa wa kazi za jeshi ni nidhamu. Huwezi kuwa askari kama huna nidhamu. Kwahiyo, mtapimwa viwango vyenu vya nidhamu” alisema Alhaj Shekimweri. Pia aliongeza kwa kusema “tafsiri ya kwanza ya nidhamu ni kuh...