Wananchi waliojiorodhesha Mkonze wawe Mabalozi kuhamasisha wengine
Na. Dennis Gondwe, BWAWANI, MKONZE WANANCHI waliojiorodhesha katika orodha ya wapiga kura wameshauriwa kuwa mabalozi ili kuhamasisha wenzao ambao hawajajiorodhesha kufanya hivyo mapema ili kuepuka foleni siku ya mwisho hatua itakayowawezesha kuchagua viongozi bora. Mkazi wa Mtaa Bwawani, Kata ya Mkonze, Patrick Richard baada ya kujiandikisha Rai hiyo ilitolewa na mkazi wa Mtaa Bwawani, Kata ya Mkonze, Patrick Richard muda mfupi baada ya kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika kituo cha Ofisi ya Afisa Mtendaji Mtaa wa Bwawani mapema leo. Richard alisema “mimi nimetumia muda mfupi sana, chini ya dakika moja kujiandikisha katika daftari la wapiga kura wakati nilijua nitatumia muda mrefu. Kumbe hata wakija watu 10 kwa pamoja watatumia chini ya dakika 10 kujiandikisha. Wito wangu wananchi waje kwa wingi kujiandikisha katika kituo hiki kilichopo kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Bwawani. Sisi ambao tumeshajiandikisha na kuona uandikishaji ulivyo tuwe mabalozi tu...