Huduma bora ni msingi wa kazi yetu
Na. Mwandishi Wetu, KIZOTA Kanda Namba Tatu yaonesha kiwango bora cha huduma kwa wateja kwa kuendelea kufanya vizuri katika kutoa huduma zinazogusa matarajio ya wananchi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja. Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Kanda Namba Tatu ya utoaji huduma katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fanuel Lawrence alipokuwa akiongelea Wiki ya Huduma kwa Mteja katika kanda hiyo. Alisema kuwa huduma bora ni wajibu wa kila mtumishi wa umma na njia ya kujenga imani na uaminifu wa wananchi kwa serikali yao. “Huduma bora ni msingi wa kazi yetu, tunapaswa kuwa na mbinu mpya, kuwa na adabu, na kujitolea ili wananchi wapate huduma stahiki” alisema Lawrence. Aidha, aliwakaribisha wananchi na wafanyabiashara katika ofisi ya Kanda Namba Tatu zilizopo katika pamoja na Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kizota kupata huduma zote muhimu. Aliongeza kuwa ofisi hizo zimesogezwa karibu na wananchi ili kuwapunguzia kero ya kufuata huduma mbali na makazi na shughuli zao. Nae, Af...