Jiji la Dodoma wahamasishwa kujiandikisha orodha ya wapiga kura
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wananchi wamehamasishwa kujitokeza kwenda kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ifikapo Oktoba 11 hadi 20, 2024 kwa lengo la kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Ushauri huo ulitolewa na Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Karama muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Kamati ya Mipango miji na Mazingira katika Shule ya Sekondari Umonja iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Karama ambae ni Naibu Meya Mstaafu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alitoa rai kwa wana Dodoma na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kushiriki katika kujiorodhesha kwenye daftari la wapiga kura kwa sababu ni muhimu kwa wananchi kutumia haki yao. Alisema kuwa kuwa uchaguzi utawasaidia kupata viongozi bora. “Uchaguzi ni gharama, hivyo serikali hugharamia chaguzi kwa ajili ya kukupa haki wewe mtanzania, ikiwa na maana wanataka uchague kiongozi unayemtaka sio uchaguliwe kiongozi” alise...