Posts

Showing posts from August 20, 2026

JIJI LA DODOMA LAITANDIKA CHAMWINO DC 38-9 MPIRA WA PETE SHIMISEMITA

Na. Mwandishi wetu, MBEYA   Timu ya Wanawake ya Mpira wa Pete ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeitandika Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino magoli 38-9 ikiwa ni muendelezo wa juhudi zake za kufukuzia ubingwa katika mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea jijini Mbeya.   Akizungumzia mchezo huo, Afisa Michezo wa Jiji la Dodoma, Neema Kilongola mara baada ya mchezo huo kutamatika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mbeya alisema kuwa timu yake imejipanga kushindana. Alisema kuwa timu hiyo inaendelea vizuri katika mashindano hayo na anaamini kuwa ubingwa wa SHIMISEMITA bado utaendelea kubaki mikononi mwao. “Tunaendelea vizuri na mashindano. Tunaamini ubingwa bado utabaki kwetu kwa sababu sisi ndio mabingwa wa mashindano haya. Hivyo, tunataka kuhakikisha tunautetea ubingwa wetu” alisema Kilongola.   Aliongezea kuwa ushindi wa magoli 38–9 umeipa Halmashauri ya Jiji la Dodoma mwanzo mzuri wa kampeni yake ya kutetea ubingwa, huku matarajio yakiongezeka kwa...