Mkuu wa Wilaya ya Dodoma atoa angalizo matumizi ya ‘Internet’ Viwandani Sekondari
Na. Nancy Kivuyo, VIWANDANI Walimu watakiwa kudhibiti matumizi mabaya ya ‘internet’ kwa wanafunzi shuleni ili kukabiliana na mabadiliko makubwa ya utandawazi na matumizi ya teknolojia. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri wakati wa Hafla ya Ugawaji wa Kompyuta na Printa kwa Shule za Sekondari za Serikali jijini Dodoma, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Viwandani. “Rai yangu ni kwamba tujitahidi kuweka ‘internet’ ili kusudi matumizi chanya kabisa ya maabara hiyo iweze kufanyika. Tukishaweka hiyo ‘internet’ tusisahau kuweka udhibiti ili vijana wetu wawe salama na matumizi yasiyo rafiki ya mitandao. Bahati mbaya wapo vijana wanaotumia mitandao kupenyeza agenda husuani mitaala ambayo haifai kwenye elimu yetu, kwahiyo ili kuzuia hayo ni muhimu kuweka vidhibiti na kuwa makini” alisema Alhaj Shekimweri. Nae, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Viwandani, Mwl. Dickson Massatu, alieleza kuwa amefurahi Shule ya Sekondari Viwandani kupatiwa vifaa hivyo kwasababu...