Na. Mwandishi wetu, MBEYA Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ya Mpira wa Pete Wanawake imeishushia kipigo kizito Timu ya Halmashauri ya Mji Ifakara cha magoli 41-3 katika siku ya pili ya Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) yanayoendelea jijini Mbeya. Mchezo huo ulianza kwa kasi katika dakika za mwanzo, lakini kadri muda ulivyokuwa ukiendelea Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilionekana kuumiliki mchezo. Hadi kufikia tamati ya mchezo huo Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliibuka na ushindi mnono wa magoli 41-3 ya Halmashauri ya Mji Ifakara. Mchezo wa Mpira wa Mikono Wanaume Halmashauri ya Jiji la Dodoma ililazimishwa sare ya 5-5 dhidi ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Aidha, katika Mchezo wa Mpira wa Kikapu ya Wanaume Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliichakaza Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa vikapu 28-7. Halmashauri ya Dodoma la Jiji iliendeleza kasi kwenye mchezo wa Mpira wa Wavu kwa Wanaume, ikiichapa Ha...