Wilaya ya Dodoma yapata “clean sheet” Miradi ya Mwenge wa Uhuru 2026
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Jumla ya miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil. 9,823,862,925 iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma imepitishwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 ili iweze kutoa huduma kwa wananchi. Miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 ni mradi wa Nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Dr. Samia-Dodoma wenye thamani ya shilingi 698,800,161, mradi wa uwekezaji binafsi wa Hoteli ya Starline wenye thamani ya shilingi 3,000,000,000 ukiwa pamoja na kutembelea mradi wa kusimika kamera za usalama wenye gharama ya shilingi 682,561,548, mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Sekondari Wella wenye thamani ya shilingi 42,800,000, mradi wa Maji safi Kata ya Nala unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira na ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilimeta 1.6 kutoka Barabara iendayo Singida hadi Hospitali ya Jiji wenye thamani ya shilingi 2,872,857,6...