Mradi wa Maji ya Mvua uliofadhiliwa na TASAF wasaidia wanafunzi Shule ya Msingi Ipala
Na. Emanuel Charles, IPALA Mwenyekiti wa Kamati ya TASAF Taifa, Peter Ilomo ameupongeza uongozi wa Kata ya Ipala kwa kuendelea kutunza miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ukiwemo mradi wa ukusanyaji maji ya mvua unaopatikana katika Shule ya Sekondari Ipala wenye lengo la kuondoa adha ya upatikanaji wa maji kwa wanafunzi shuleni hapo. Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa na TASAF, Ilomo alisema kuwa lengo la kwenda kukagua mradi huo ni kuangalia kama unafanya kazi na kusaidia wanafunzi kama ilivyokusudiwa. āTunashukuru mradi ulianza 2022 na kumalizika 2023, kwakuwa tayari mradi umeshakamilika na jamii inayozunguka mradi huu kwa maana ya wanafunzi na waalimu wananufaika tunasema asante sana. Lengo lakuja hapa ni kukagua kama mradi unafanya kazi kwasababu mara nyingi miradi unaweza kukamilika lakini usifanye kazi, nipongeze uongozi wa hapa Ipala, ninyi mmekuwa wa tofautiā alisema Ilomo. Pia aliongeza kwa kusema ...