Posts

Showing posts from February 17, 2025

Dodoma Jiji FC, Fiti Kuwavaa Wajelajela

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, imejiandaa kuwakabili Klabu ya soka ya Tanzania Prisons katika muendelezo wa mbilinge mbilinge za duru ya pili ya Ligi kuu ya NBC Tanzania bara hapo kesho katika dimba la Jamhuri Dodoma. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Tanzania Prisons, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji FC,   Meck Mekisime alisema “Timu ipo tayari na tumejiandaa vizuri tukijua kuwa mchezo utakua mgumu kwasababu wapinzani wetu wametoka kupoteza michezo miwili mfululizo. Kwahiyo, sisi kama klabu tupo tayari kupambana na kuhakikisha alama tatu zinabaki Dodoma na niwaombe mashabiki na wanadodoma kwa ujumla kesho waje kwa wingi uwanjani kuja kuwaunga mkono wachezaji na kuwafariji kutokana na kile kilichotokea siku kadhaa zilizopita, jambo ambalo litawaongezea nguvu wachezaji kuipambania timu huku wakijua kuna namba kubwa ya watu jukwaani inawaunga mkono”. Nae, Augustin Nsata, Nahodha wa klabu ya Dodoma Jiji FC, akaelezea hali y...