Dodoma Jiji U20 yatuma salamu Ligi ya Vijana
Na Mussa Richard, DODOMA Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji chini ya umri wa miaka 20 imetuma salamu kwa timu zinazoshiriki ligi ya vijana ya NBC chini ya miaka 20 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Tabota United chini ya miaka 20 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma hapo jana. Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha mkuu wa timu hiyo, Chido Jeremiah alisema “tunamshukuru Mwenyezi Mungu mchezo umeisha salama na tumepata ushindi wa magoli mengi na ushindi wa kutuheshimisha na kutuweka mbele zaidi na wanaotufuata. Japo hatukua na mchezo mzuri kipindi cha kwanza lakini wakati wa mapumziko tukawapa vijana maelekezo ya kufanya kutokana na mapungufu tuliyoyaona kwa wapinzani wetu ndiyo maana tuliporudi kipindi cha pili tukafanikiwa kupata mabao manne. Kwa upande wa timu imeendelea kuimarika na vijana wameanza kujituma na niwashukuru mashabiki wamejitokeza kuiangalia timu yao na wameona jinsi inavyocheza. Kwahiyo, niwaombe wanadodoma wasiiache timu hii timu ni ...