Posts

Showing posts from January 31, 2025

Dodoma Jiji FC inafukuza Mwizi Kimya Kimya

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA Timu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, imeendelea na maandalizi ya kujiwinda na michezo ya Ligi kuu ya NBC Tanzania bara, kwasasa imekita kambi mkoani Arusha, na imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Mbuni FC, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha na Dodoma Jiji FC kuchomoza na ushindi wa bao 1-0. Akizungumza baada ya mchezo kutamatika Kocha wa Viungo wa Dodoma Jiji FC, Fransis Mkanula alisema “tumekuja hapa Arusha kuweka kambi ya siku tano, tumekuja hapa kupata mechi za kirafiki kwasababu timu imetoka kwenye mapumziko, baada ya ratiba kutoka tukaamua kuja hapa Arusha kucheza mechi za kirafiki ili kurudisha utimamu wa miili kwa wachezaji pia ukizingatia tuna maingizo mapya kwenye timu. Kwahiyo, tumekuja kutengeneza mazingira ya kuzoeana na wenzao na kuingia kwenye mfumo wa timu”. Nae, Nahodha wa Dodoma Jiji FC, Augustin Nsata akaelezea hali ya kambi na maandalizi ya timu kuelekea kwenye michezo ...

Dodoma Jiji U20 FC yakamiwa na Maafande wa Gunners FC

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA Timu ya soka ya Dodoma Jiji chini ya umri wa miaka 20 imechezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Timu ya Gunners FC, katika mchezo wa kirafiki uliovurumishwa katika uwanja wa Shell Complex jijini Dodoma hii leo. Akizungumza baada ya kutamatika kwa dakika tisini Kocha Mkuu wa Timu ya Dodoma Jiji U20, Jeremiah Chido alisema “mchezo umeisha salama, tumepoteza mchezo kwasababu tumekutana na timu nzuri na yenye daraja la juu. Kwetu sisi alikuwa ni mshindani sahihi kutokana na maandalizi yetu tunayoyafanya kwaajili ya michezo inayofuata ya ligi ya vijana michezo ambayo tutakuwa ugenini ndiyo maana leo tumewapa nafasi wachezaji wote ili kuwatengenezea utimamu wa mwili kwaajili ya kurudi kwenye michezo ya ligi’’. Katika hatua nyingine Chido akazungumzia hali ya majeruhi kwenye timu yake na kuwaaminisha mashabiki kuwa wachezaji hao watarejea uwanjani na kuendelea kuipambania timu. “Katika mchezo wa leo wachezaji wawili wamepata majeraha, lakini siyo majeraha makubw...

Kata 41 jijini Dodoma kunufaika na Milioni 150 za Miradi ya Maendeleo

Image
Na. Shahanazi Subeti, DODOMA Baraza la Madiwani wa Jiji la Dodoma wameipongeza Halmashauri ya Jiji chini ya Mkurugenzi na jopo lake kwa kutenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya kumalizia miradi viporo na shilingi milioni 150 kwa kila kata kuanzisha miradi mipya ili kuleta maendeleo kwa wananchi. Madiwani waliyasema hayo katika mkutano maalum wa kupitia rasimu ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, alisema kuwa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inalenga kukamilisha miradi viporo katika jumla ya kata 41 za halmashauri hiyo. “ Kwa mwaka huu, Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inafikia takribani shilingi Bilioni 147 inayolenga kwenda kukamilisha miradi viporo katika kata zetu 41. Miradi yote ambayo haikuisha kwa wakati kutokana na sababu zozote zile. Hivyo, tayari imetengwa kiasi cha shilingi Bilioni saba ili ...

Jiji la Dodoma kuingia ubia utekelezaji Miradi

Image
  Na. Halima Majidi, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika kuhakikisha inaimarisha na kukuza wigo wa ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo yake na nchi kwa ujumla imeainisha miradi ya kuingia ubia na kushirikisha sekta binafsi na za umma. Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupitia mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2025/2026, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Prof. Davis Mwamfupe, alisema kuwa halmashauri imekuja na mkakati mpya wa kujiweka tayari kwa kufanya miradi kwa ubia kupitia mfumo wa ushirikishaji sekta binafsi na sekta ya umma (PPP). Prof. Mwamfupe alisema kuwa miradi mingi imewekwa katika masoko ili kuweza kuita na kuvutia sekta binafsi ili waweze kushiriki na kuwekeza katika miradi hiyo. “Kwa kuangalia miradi ambayo tulikuwa nayo kipindi cha nyuma na kwa kujifunza kutokana na hiyo tumepata tabu sana kukamilisha miradi miwili ya hoteli. Kwahiyo, tumeweka mkaka...