Waganga Wafawidhi wa Jiji la Dodoma wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa NeST
Na. Halima Majidi, DODOMA Waganga wafawidhi kaitka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamewezeshwa mafunzo ya ununuzi kwa njia ya mfumo serikalini ‘National e- Procurement System of Tanzania’ (NeST) yatakayoongeza ufanisi na kurahisisha utendaji wa kazi pamoja na kupunguza hoja za ukaguzi kwa sababu kila kitu kitakuwa kipo wazi. Mafunzo hayo yalitolewa na Kitengo cha Manunuzi na Ugavi cha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa lengo la kuongeza ufanisi, kupunguza gharama pamoja na kuokoa muda, ambayo yalifanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga. Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Josephat Nyumayo, alieleza kuwa, mafunzo hayo yalikuwa yanahusu matumizi ya mfumo wa ‘NeST’ katika ngazi ya kata kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2023 na Kanuni zake za Mwaka 2024, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali kuwa manunuzi yote yafanyike kwa mfumo huo. Aidha, Nyumayo alisema kuwa, mafunzo hayo ni ya awamu ya pili kwa waganga wafawidhi ambapo mafunzo ya awali yalikuwa yanahusu matumi...